MTIBWA SUGAR WATAMBA KUIFUNGA MBAO FC

 Uongozi wa timu ya soka ya Mtibwa Sugar ya Manungu Turiani,mkoani Morogoro umesema kwamba kikosi chao kimejipanga vyema kuwakabili Mbao FC ya Ilemela kutoka jijini Mwanza katika mechi yao ya ligi kuu ya Tanzania bara inayotaraji kupigwa siku ya jumamosi kwenye mashamba ya miwa.

Msemaji wa Mtibwa Sugar Tobiasi Kifaru amesema kikosi kinaendelea vyema na maandalizi chini ya kocha mkuu Salum Mayanga na dhumuni kubwa ni kufanya vizuri kwenye pambano hilo.

Amesema kwamba uongozi unatambua kua pambano hilo linataraji kua na ushindani mkubwa hasa kutokana na hamasa waliyonayo timu ya Mbao baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Ruvu Shooting tena wakiwa ugenini lakini jambo hilo haliwapi hofu.

No comments