DTB YATOA MILIONI 250 KUDHAMINI LIGI KUU YA TANZANIA BARA
Benki ya Daimond Trust leo hii imesaini mkataba na TFF kwa kudhamini ligi kuu ya Tanzania bara kwa msimu wa mwaka 2016/2017 wenye thamani ya shilingi milioni 250.
Akiongea mbele ya waandishi wa Habari leo hii Raisi wa TFF,Jamali Malinzi ameishukuru kampuni hiyo binafsi kwa kujikita kwenye michezo kwani udhamini wao utakua na tija kwa upande wao na hii inatokana na TFF kutokua na uwezo wa kuzihudumia timu za taifa kutokana na kukosa udhamini wa kutosheleza mahitaji yao.
Malinzi amesema kwamba kwa muda mrefu TFF imekua ikifanya jitihada kubwa kuhakikisha wanapata wadhamini ambao watazisaidia klabu ili navyo viweze kujikimu kwenye maswala ya uendeshaji kwani kwa sasa mapato ya viwanjani yameshuka hivyo ni vigumu kwa TFF na vilabu ambavyo havina wadhamini kujiendesha kwa weledi.
"Ukweli ni kwamba kwa sasa mapato ya viwanja yameshuka mfano mzuri tu ni mechi ya Azam na Simba TFF tumeambulia milioni mbili pekee kutokana na mgao wetu siwezi kuzungumza sana sababu za kushuka kwa mapato kwani nadhani wengi mnazifahamu sababu hizo"alisema Malinzi.
Post a Comment