NAPE AZINDUA RASMI TIKETI ZA ELEKTRONIC,SIMBA NA YANDA KUANZA KUTUMIA MFUMO HUO

Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Nape Nnauye leo hii amezindua rasmi mfumo wa tiketi za Elektronic ambao kwa mujibu wa taarifa yake ni kwamba tiketi hizo zitaanza kutumika katika mchezo wa watani wa jadi Simba na Yanga ikiwa ni mechi ya ligi kuu ya Tanzania bara inayotaraji kupigwa siku ya oktoba moja mwaka huu.

Akiongea mbele ya waandishi wa Habari leo hii uwanja wa taifa jijini Dar es salaam,Nape amewataka wadau wa mpira wa miguu hapa nchini na wahusika wa mfumo huo kua makini kwani kusije kuleta athari ambayo ikaja kuwapa nguvu wanaopingana na mfumo huo.

Amesema kwamba si kila mmoja anaefurahia mchakato huo kwani baadhi yao ambao wamekua wakipata manufaa hapo nyuma hawatapenda kuona swala hilo likifanikiwa kwani litaziba mianya ya kujinufasha wao wenyewe.

No comments