SIMBA WASEMA MECHI YA MAJIMAJI NI NGUMU KULIKO MECHI YAO NA YANGA

Wakati homa ya pambano la watani wa jadi Simba na Yanga ikiendelea kutawala kona mbalimbali kwa mashabiki wa klabu hizo kongwe hapa nchini,leo hii mwenyekiti wa tawila la Simba lijulikanalo Mpira Pesa Ostadhi Masudi amesema kwamba kwa upande wao wao hawana hofu na pambano hilo bali kilichopo kwa sasa wameelekeza nguvu zao kwenye pambano lao dhidi ya Majimaji likalopigwa siku ya jumamosi kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.

Akiongea na MWANDIKE.BLOGSPORT,Masudi amesema kwamba kwa sasa hawana mpango wa kufikilia mechi ya Yanga kwa kua timu hiyo ni ya kawaida na mara nyingi wamekua wakiifunga mara kwa mara.

"Msimu uliopita Yanga walitufunga kwa kubahatisha lakini wao hawana ubavu wa kutufanga kila wakati,Yanga kwetu ni watu wa kujipigia tushawafunga goli sita pia tushawafunga goli tano bila na wameshawai kutukimbia uwanjani kwa hiyo hatuna presha nao"alisema Masudi.

Amesema kwamba mechi yao inayofuata dhidi ya Majimaji ni mechi ngumu kuliko ya Yanga kwani wapinzani wao hawatakubali kufungwa kirahisi baada ya timu hiyo kutokua na matokeo mazuri tangu kuanza kwa ligi kuu ya Tanzania bara.

No comments