MGOSI ASEMA SWALA LA IBRAHIMU AJIBU KUCHEZA KESHO AU KUTOCHEZA LIPO KWA KOCHA MKUU

Meneja wa timu ya soka ya Simba Musa Hassani Mgosi amesema kwamba kikosi cha timu hiyo kimejipanga vyema kuwakabili timu ya Majimaji hapo kesho katika mchezo wa ligi kuu ya Tanzania bara unaotaraji kupigwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Mgosi amesema kwamba wachezaji wote wapo vizuri hivyo wanataraji kuingia kwenye pambano hilo wakiwa na hamasa kubwa ya kupata matokeo mazuri.

Amesema kwamba mechi ya kesho itakua ngumu kwa upande wao kutokana na wapinzani wao nao kuhitaji ushindi hasa baada ya kufanya vibaya katika michezo yao iliyopita.

Katika hatua nyingine Mgosi amesema kwamba kwa upande wao hawafikilii kutomtumia mchezaji Ibrahimu Ajibu kwa kua ana kadi mbili za njano ispokua kama atakua katika programu ya mwalimu basi atakua miongoni mwa wachezaji watakaocheza kwenye pambano hilo dhidi ya Majimaji.

Mgosi amesema kwamba hawawezi kukosa kumpanga Ajibu eti kisa ana kadi mbili za njano ambazo zitamuweka kwenye mazingira magumu endapo atapewa kadi nyingine ya njano atashindwa kucheza mechi inayofuata dhidi ya Yanga.

Amesema kwamba endapo kutafanyika swala hilo kunaweza kuleta athari kubwa kwa wachezaji wenzake kwani kutakua na mataba ya wachezaji kwa kuona kua wengine hawasaminiki.

No comments