KILIMANJARO QUENS KUTINGA BUNGENI MKOANI DODOMA



Serikali ya Tanzania kupitia kwa Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo  wameipongeza timu ya wanawake ya Tanzania bara Kilimanjaro Quens kwa kufanikiwa kuwa mabingwa wa kwanza katika michuano  iliyoandaliwa na  CECAFA baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Kenya.

Akiongea na MWANDIKE BLOGSPORT, Waziri wa habari,utamaduni,Sanaa na Michezo Nape Nnauye amesema kwamba kwa upande wa Serikali wamefarijika na ushindi huo wa Kilimanjaro Quens kwani umeonyesha chachu ya mafanikio katika nchi yetu.

Amesema kwamba kwa kutambua umuhimu wao wana mpango wa kuwaalikia bungeni katika bunge lijalo kwa ajili ya kuwapa pongezi na pia kupata fursa ya kucheza mpira wa miguu na wabunge wanawake mkoani Dodoma.

No comments