TFF YAZISHUSHA DARAJA KWA MARA NYINGINE POLISI TABORA NA GEITA GOLD

Polisi Tabora na Geita Gold hazitashiriki kucheza ligi daraja la pili msimu huu baada ya klabu hizo kushindwa kukamilisha zoezi la usajili wa wachezaji hadi dirisha lilipofungwa.

Ofsa Habari wa TFF,Alfred Lucas amesema kwamba timu hizo ambazo zilishushwa daraja kutoka daraja la kwanza hadi ligi daraja la pili kwa kosa la kujihusisha na upangaji wa matokeo zimeshindwa kukamilisha zoezi hilo hivyo timu hizo hazitapata fursa ya kucheza ligi hiyo.

Amesema kwamba mbali na kutoshiriki ligi pia timu hizo zimeshushwa daraja kwa kufuata kanuni na misingi ya ligi daraja la pili kufuatia timu hizo kushindwa kushiriki ligi hiyo ya daraja la pili.

No comments