YANGA WATOA UFAFANUZI JUU YA MAOMBI YA MCHEZAJI ADAM SALAMBA

Na Said Ally
Mwenyekiti wa kamati ya usajili Yanga,Hussein Nyika amesema kwamba klabu hiyo ipo katika mpango wa kumsajili mchezaji Adam Salamba kutoka Lipuli FC kwa ajili ya kuisadia timu kwenye michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika.

Nyika ameiambia MWANDIKE BLOG kuwa Yanga kwa sasa haiwezi kuomba mchezaji kama inavyoelezwa na baadhi ya wadau bali klabu hiyo ikihitaji mchezji inasajili moja kwa moja.

Alisema kwamba wao kama uongozi wameiomba Lipuli kutaka kumsajili Salamba kwani mchezaji bado angali na mkataba wa kuwatumikia Wanapaluhengo hao wa mkoani Iringa.

Aidha alisema kwamba swala hilo litakapokamilika wao kama uongozi utaliweka wazi kwa wanachama na mashabiki wa Yanga.

Hata hivyo aliongeza kwa kusema kwamba mbali na Salamba lakini pia uongozi upo katika mazungumzo na baadhi ya wachezaji kwa lengo la kutaka kuwasajili.

No comments