KAHEZE ATHIBITISHA RASMI KUJIUNGA NA SIMBA

Mshambuliaji wa timu ya Majimaji Marcel Kaheze amethibitisha rasmi kusaini kandarasi ya kuitumikia klabu ya Simba katika msimu ujao wa ligi kuu ya Tanzania bara.

Kaheze ameiambia MWANDIKE BLOG kwamba yeye kama mchezaji ana wajibu wa kuicheza timu yeyote ambayo anaona inaafaa hivyo kwa sasa mashabiki wanapaswa kutambua jambo hilo.

Mchezaji huyo alikuwa miongoni mwa wachezaji tegemeo katika kikosi cha timu ya Majimaji FC,ambacho leo hii kimeshuka daraja rasmi baada ya kutoka sale ya bao 1-1 na timu ya Simba huku yeye akipachika bao la kuongoza kwa timu yake.

No comments