RASMI:SALAMBA ASAJILIWA SIMBA


Simba imefanikiwa kukamilisha usajili wa mchezaji Adam Salamba aliyekuwa anaitumikia timu ya Lipuli FC ya mkoani Iringa kwa ajili ya kuitumikia timu hiyo katika msimu ujao wa ligi kuu ya Tanzania bara na michuano ya kimataifa.

Awali Salamba alikuwa anahusishwa kutaka kujiunga na klabu ya Yanga ambayo uongozi wake uliwahi kuwasilisha barua ya maombi ya kumuhitaji mchezaji huyo ili awasaidie kwenye michuano ya kimataifa.
Mbali na Yanga, pia mchezaji huyo alikuwa anahusishwa kutakiwa na klabu ya Azam FC ambayo nayo ni miongoni mwa timu zilizokuwa zikielezwa kuhitaji huduma yake.


No comments