KAHEZA AWAOMBA RADHI SIMBA

Mchezaji Marcel Kaheza amewaomba radhi mashabiki wa timu ya soka ya Simba baada ya kuifungia timu ya Majimaji bao la kuongoza katika mchezo wa ligi kuu ya Tanzania bara uliomalizika kwa sale ya bao 1-1.

"Naombeni mnisamehe mafans wangu wa Simba mechi haikuwa na umuhimu kwenu kama ubingwa tayari.Nawapenda"aliandika Kaheza kupitia ukurasa wake wa instagram.

Hata hivyo mchezaji huyo tayari amethibitisha kusajiliwa na klabu ya Simba hivyo msimu ujao ataonekana katika kikosi cha mabingwa wa ligi kuu ya Tanzania bara.

No comments