BAADA YA KUSAINI SIMBA,SALAMBA AONEKANA NA GARI JIPYA

Baada ya kusaini kandarasi ya miaka miwili katika klabu ya Simba,mchezaji Adam Salamba leo hii amepiga picha akiwa na gari mpya.

Salamba amejiunga na klabu ya Simba akitokea Lipuli FC,huku ikielezwa amesaini kwa dau la shilingi milioni 40.

Awali Salamba alikuwa anahusishwa kutaka kujiunga na klabu ya Yanga ambayo uongozi wake uliwahi kuwasilisha barua ya maombi ya kumuhitaji mchezaji huyo ili awasaidie kwenye michuano ya kimataifa.

Mbali na Yanga, pia mchezaji huyo alikuwa anahusishwa kutakiwa na klabu ya Azam FC ambayo nayo ni miongoni mwa timu zilizokuwa zikielezwa kuhitaji huduma yake.

No comments