YANGA YAENDA KENYA BILA YONDANI
Na,Said Ally
Mchezaji Kelvin Yondani hatosafiri na kikosi cha timu ya Yanga kinachotaraji kuelekea nchini Kenya hapo kesho kwa ajili ya kushiriki michuano ya SportPesa Super Cup.
Jumla ya wachezaji 20 na viongozi saba wa timu ya Yanga hapo kesho wataelekea nchini Kenya kwa ajili ya kushiriki michuano hiyo ya SportPesa lakini katika orodha ya wachezaji hao jina la Kelvin Yondani halipo.
Mwenyekiti wa kamati ya usajili Yanga,Hussein Nyika alisema kwamba Yondani atakosekana katika kikosi hicho kwa sababu hayupo vizuri baada ya kuumia kabla ya kufungiwa na TFF.
Nyika alisema kwamba kabla ya kufungiwa na TFF,Yondani alikuwa anacheza huku akiumwa kutokana na uvimbe chini ya goti hivyo baada ya kufungiwa na TFF kwake alipata wakati mzuri wa kupumzika lakini hadi sasa bado hayupo vizuri.
Aidha alisema kwamba yeye binafsi ameshauri Yondani apumzike safari hiyo ili aweze kupona vizuri na kisha kuitumikia Yanga katika michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika.
Hata hivyo alisema kwamba kwa sasa mchezaji huyo kandarasi yake inafikia ukingoni june 30 mwaka huu lakini uongozi ushaanza mikakati ya kumpa mkataba mpya.

Post a Comment