YANGA KUIFUATA DICHA HAPO KESHO

KIKOSI cha Yanga Sc  kinatarajia kuaondoka  jumapili alfajili kueleka Ethiopia tayari kwa mchezo wa marejeano wa kombe la shirikisho dhidi ya wenyeji Welayta Dicha Sc,mchezo uliopangwa kuchezwa jumatano ya tarehe 18 april kwenye mji wa  Hawassa.

Muda mfupi uliopita meneja wa kikosi  Hafidh Saleh amesema kuwa  Yanga inasafiri kueleka Ehtiopia ikiwa na matuamini makubwa ya kupata ushindi na kufanikiwa kuingia kwenye hatua ya makundi,licha ya changamoto kadhaa ambazo kikosi chake kinapitia kwa sasa.

"Ziko changamoto kadhaa tunapitia kwa sasa kama klabu,lakini tunayo matumaini mkaubwa ya kucheza vizuri na kupata mataokeo,nia ya kila mmoja ni kuhakikisha tunasonga mbele,tunafahamu ubora wa wapinzani wetu na umuhimu wa mchezo tunaokwenda kucheza,ushindi na kufanikiwa kufuzu kwa hatua ya makundi ndiyo jambo pekee  ambalo litakuwa faraja ya kila mmoja wetu"alisema Hafidhi.

Akiendelea zaidi Hafidh ametanabaisha kuwa jumla ya wachezaji 20 na viongozi 11 wakiwemo 7 wa benchi la ufundi  na wengine  watatu kutoka ndani ya sekretarieti ya Yanga wataungana na Athumani Nyamlani kutoka shirikisho la soka nchini ambaye pia ndiyo atakuwa kiongozi wa msafara mzima.

orodha kamili ya wachezaji pamoja na viongozi kutoka benchi la ufundi,itatangazwa hapo kesho.

No comments