WANACHAMA YANGA WAUTAKA UONGOZI UONDOKE MADARAKANI

Na,Said Ally
Katibu mkuu wa Tawi la Yanga,Tandale kwa Mtogole Waziri Jitu amewataka viongozi wa klabu hiyo chini ya makamu mwenyekiti Clement Sanga kuondoka ndani ya klabu kwa kuwa wameshindwa kuiendesha timu kwa weledi.

Jitu ameiambia MWANDIKE.BLOGSPORT,kwamba viongozi hao wanapaswa kuondoka na kuwaachia timu yao kwani anaamini uendeshaji wa timu umeshawashinda.

Alisema kwamba kwa mwenedo uliopo hivi sasa hasa baada ya matokeo ya jana katika mchezo dhidi ya Singida United,mechi iliyomalizika kwa timu hizo kufungana bao 1-1 inaonyesha wazi kuwa ndani ya Yanga hakuna utendaji mzuri.

Aidha Jitu ameitaka serikali kuingilia kati swala la kuitisha uchaguzi wa klabu ili kujaza nafasi iliyoachwa wazi na  aliyekuwa mwenyekiti wa klabu Yusuf Manji.

Hata hivyo aliongeza kwa kusema kwamba endapo kama serikali itashindwa kuchukua jukumu la kuiongoza Yanga ifanye uchaguzi,basi ana imani siku chache zijazo kutatokea mgogoro mkubwa kama ule uliomuondosha Jamali Malinzi wakati akiwa kiongozi wa Yanga.

No comments