TANZANIA YAPANDA KWENYE VIWANGO VYA FIFA

Tanzania imepanda kwa nafasi 9 kwenye nafasi za ubora wa viwango vya FIFA kutoka nafasi ya  146 hadi 137.

Kupanda kwa Tanzania kumetokana na kufanya vizuri katika mchezo wa kirafiki dhidi ya DR Congo ambao licha ya kufungwa lakini wamefanikiwa kupanda kwa nafasi moja kutoka 39 hadi 38.

Uganda wameendelea kuongoza katika ukanda wa Afrika Mashariki wakipanda kwa nafasi 4 kutoka 78 hadi 74.

Kenya imekamata nafasi ya 113 ikiporomoka kwa nafasi 8 kutoka 105.

Ugerumani imeendelea kushika namba moja Duniani ikifuatiwa na Brazili,Belgium,Ureno na Argentina.

Tunisia imeshika nafasi ya kwanza katika bara la Afrika ikipanda kwa nafasi 9 kutoka nafasi ya 23 hadi 14.

No comments