MTIBWA SUKARI WAMPA MKATABA MPYA KINDA WA NGORONGORO HEROES

Na Said Ally
Kinda wa klabu ya Mtibwa Sugar Kibwana Ally Shomary na timu ya taifa ya vijana Ngorongoro Heroes amesaini mkataba wa kuendelea kukitumikia kikosi cha wana tam tam.
Mtibwa Sugar pamoja na Kibwana Ally Shomary wamefikia makubaliano ya kuingia kandarasi ya miaka miwili hivyo mkataba wake utakuwa wa misimu miwili na misimu hiyo ni 2018/2019, 2019/2020.
Kibwana Shomary anayemudu kucheza beki wa pembeni wa kulia alikuwa ameitumikia Mtibwa Sugar kwa miaka miwili na mwaka wake wa pili ulikuwa unaelekea mwishoni.
Msemaji wa Mtibwa Sugar,Thobias Kifaru amesema kwamba uongozi umeamua kumpa kandarasi Shomari baada ya kurishwa na kiwango chake pamoja na nidhamu yake klabuni hapo.
Alisema kwamba si mchezaji huyo pekee bali klabu hiyo itaendelea na mchakato huo wa kuwapa mikataba wachezaji wao vijana ambao wanaonekana wana uwezo wa kuisaidia Mtibwa Sugar.
Kibwana Ally Shomary alianza kutumikia kikosi cha timu ya Mtibwa Sugar ya vijana (Academy) tangu mwaka  2016 na mwaka huu tarehe 6.04.2018 alianza kutumikia kikosi cha timu ya wakubwa katika mchezo dhidi ya Singida United na Mtibwa ili ibuka na ushindi wa goli 3-0 na baadae alicheza mchezo wake wa pili dhidi ya Simba tarehe 9.04.2018 na Mtibwa ilipoteza kwa goli 1-0, michezo yote miwili Kibwana alionesha kiwango kizuri.

No comments