SINGIDA UNITED YAWASILI DAR NA WACHEZAJI 21

Na Said Ally
Kikosi cha timu ya Singida United jioni hii kimetarajiwa kuwasili jijini Dar es salaam tayari kwa ajili ya mchezo wao wa ligi kuu ya Tanzania bara dhidi ya Yanga.

Meneja wa timu hiyo Ibrahimu Mohammed ameiambia MWANDIKE.BLOGSPOT kwamba Jumla wa wachezaji 21 na viongozi 7 wa kikosi hicho wanawasili jijini Dar es salaam tayari kwa ajili ya kujiwinda na pambano hilo litakalopigwa siku ya jumatano kwenye uwanja wa Taifa.

Mohammed alisema kwamba kikosi hicho kinataraji kufanya mazoezi ya mwisho siku ya kesho kabla ya kungia uwanjani.

Aidha alisema kwamba mechi yao dhidi ya Yanga itakuwa ngumu lakini kwao wamejipanga kupata matokeo mazuri hasa baada ya kutokuwa na bahati ya kupata ushindi kwenye uwanja wa Taifa kwa mechi za hivi karibuni.


No comments