UONGOZI MPYA WA MPIRA WA MEZA USO KWA USO NA MRAJIS
Na Sleiman Ussi,Zanzibar
Uongozi mpya wa Chama cha Mpira wa Meza Zanzibar “Zanzibar Table Tennis Association (ZTTA)” umekutana uso kwa uso na Mrajis wa Vyama vya Michezo Visiwani Zanzibar Suleimana Pandu katika Ofsi yake iliyopo Baraza la Taifa la Michezo Zanzibar (BTMZ) Mwanakwerekwe Mjini Unguja.
Afisa Habari wa Chama hicho Abubakar Khatib Kisandu alisema kwamba lengo kuu la kukutana nae ni kutambuana baada ya viongozi wa chama hicho kupata haki ya kukiongoza chama hicho.
Alisema kwamba tangua viongozi wa chama hicho walipoingia madarakani walikuwa hawajakutana na mrajisi wa vyama vya michezo Zanzibar,hivyo kukutana ne ni jambo ambalo wamelifurahia zaidi kwa upande wao kwani wanaamini kuitwa kwao na kiongozi huyo ni jambo kubwa kwa maendeleo ya mchezo huo.
Agost 6, 2017,Chama cha Mpira wa Meza Zanzibar “Zanzibar Table Tennis Association (ZTTA)” kilipata viongozi wapya, Viongozi ambao wataongoza kwa muda wa miaka 4 ijayo ndipo utafanyika uchaguzi mwingine kwa mujibu wa katiba ya Chama hicho.
Viongozi hao 7 ni Latifa Daud Jussa Mwenyekiti, Makamo Mwenyekiti ni Faki Ali Faki, katibu Ahmed Abdallah, katibu msaidizi Omar Mohd Othman, Asha Haji Ame mhasibu mkuu, Abubakar Khatib Haji (Kisandu) Msaidizi Mhasibu huku Salum Ramadhan Abdallah ni mjumbe.
Post a Comment