MANARA AKELWA NA KITENDO CHA MASHABIKI KUMTUKANA

Mkuu wa idara ya Habari na mawasiliano wa klabu ya Simba,amewalaumu mashabiki wa mpira kwa kitendo chao cha kumtukana kupitia mitandao ya kijamii.

Manara alisema kwamba kitendo hicho ambacho kinafanywa na mashabiki si cha kiungwana na serikali inatakiwa kuchukua hatua kali kwa wahusika.

"Sijui kosa langu nililolifanya nimeambiwa nimemwambia mchezaji wao sijui Tshishimbi kafanana na Shilole,mimi mshabiki wa Simba ukiachana na cheo changu lakini sikuandika kitu kibaya zaidi ya kumlaumu Shilole kwa jambo aliloliandika kuhusu kutumia jina lake kwa mchezaji Tshishimbi"alisema Manara.

Alisema kwamba mashabiki hao wanapaswa kubadilika kwani ushabiki si uwadui kama inavyochukuliwa na baadhi yao.

No comments