MANJI ADAI YEYE BADO DIWANI WA KATA YA MBAGALA KUU

Na Unique Maringo
Aliyekuwa mwenyekiti wa klabu ya Yanga na Diwani wa Kata ya Mbagala kuu Yusufu Manji,ameiambia Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu Kuwa hatambui kuvuliwa udiwani  hivyo yeye bado anatambua kuwa ni diwani wa kata ya Mbagala Kuu.

Manji ametoa malalamiko hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Huruma Shahidi wakati alipo hudhuria kesi yake ya Uhujumu UChumi inayomkabili.

Mbele ya Hakimu Shahidi Manji amedai kuwa amezipata taarifa za kuvuliwa udiwani kupitia magazeti na hatambui kuvuliwa udiwani.

"Sijui kama ni kweli nimevuliwa udiwani,mimi ninalo gazeti la mwananchi Mkononi ambalo nimepata taarifa kwao, 
ni miezi miwili sasa niko mahakamani,kabla sijaja mahakamani nilikua nahudhuria vikao vyote vya vyama na halmashauri.

Mimi silaumu Gazeti la Mwananchi.Ninachoomba ni Mahakama kwakua inajua uzito wa kesi hii 
Mahakama iagize DPP Aiambie halmashauri ya Manispaa ya Temeke kwamba wao ndo wamenikamata na ndiomaana sihudhurii kwenye vikao vya hamashauri"alisema Manji.

Ameongeza kuwa kama wakitaka ahudhurie vikao hivyo DPP atoe hati ya kutolewa gerezani aende kwenye vikao.
au wamuandikie barua itakayo onyesha agenda zenyewe na yeye ajibu  kwa njia ya maandishi.

Amesisitiza Mahakamani hapo mimi ni diwani na natambua kuwa ni  Diwani wa kata ya mbagala Kuu na kama nimevuliwa au sijavuliwa udiwani mimi sitambui,Mimi nimeshatumia zaidi ya shilingi million 70,na hii yote nimetoa kwenye mfuko wangu kwa lengo la kusaidia maendeleo katika Kata yangu ya Mbagala Kuu na sio mfuko wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke.

Aidha hakimu Huruma Shahidi alisema DPP anatakiwa ashughulikie madai hayo.

Awali Wakili wa Serikali Mutalemwa Kishenyi aliambia Mahakama kua,shauri hilo limekuja mahakamani kwa ajili ya kutajwa na upelelezi haujakamilika na kuomba tarehe ya kutajwa ambapo Wakili wa Manji Seni Malimi ameomba mahakama ahirisho la karibu ambapo shauri hilo litatajwa sept 18 2017.

Washtakuw katika keso hiyo uhujumu uchumi ni Meneja rasilimali watu wa kampuni ya Quality Group ltd Deogratias kisinda,Tobias Fwere  na Abdala Sengei,kwapamoja na Yusufu Manji wanakabiliwa na mashtaka ya uhujumu uchumi.

Manji na wenzake wamerudishwa rumande kwakua mashtaka yauhujumu uchumi yanayo wakabili hayana dhamana.

No comments