GEORGE LWANDAMINA AKASIRISHWA NA RATIBA YA LIGI KUU

Uongozi wa klabu ya Yanga umesema kwamba kikosi cha timu hiyo kinaendelea na mazoezi kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wao wa siku ya jumapili dhidi ya Njombe Mji.

Afsa Habari msaidizi wa Yanga,Godlsten Anderson Chicharito alisema kwamba kuelekea kwenye mchezo huo kocha mkuu George Lwandamina amehudhunishwa na mabadiliko ya ratiba ambayo amedai yameharibu mipango yake.

Alisema kwamba kocha alikuwa na mipango yake tofauti ambayo aliipanga,lakini sasa baada ya mabadiliko hayo ya ratiba itambidi afanye mabadiliko mengine katika programu zake.

Aidha alisema kwamba baada ya mazoezi ya kesho uongozi utaweka bayana juu ya safari yao ya kuelekea Njombe kwa ajili ya mechi hiyo ya ligi kuu Tanzania bara.

No comments