SIMBA WATAMBA KUIFUNGA AZAM FC KWENYE UWANJA WAO

Uongozi wa klabu ya Simba umesema kwamba kikosi cha timu hiyo kipo tayari kwa ajili ya mchezo wao wa ligi kuu ya Tanzania bara dhidi ya Azam FC,mchezo unaotarajiwa kupigwa siku ya jumamosi katika uwanja wa Azam Complex ulioko Chamazi.

Mkuu wa idara ya Habari na mawasiliano wa klabu ya Simba,Haji Manara alisema kwamba wahezaji wote waliopo kambini wako vizuri na kila mmoja ana hamasa ya kufanya vizuri kwenye pambano hilo.

Alisema kwamba wachezaji wao wa kimataifa Juuko Murshid na Emmanuel Okwi wanatarajiwa kuwasili hapa nchini leo hii wakati wowote kuanzia sasa.

Aidha alisema kwamba kuelekea kwenye pambano hilo wataendelea kukosa huduma za wachezaji wao wawili ambao ni mlinda mlango Said Mohamed anaetarajiwa kupelekwa nchini India kwa ajili ya matibabu pamoja na beki Shomari Kapombe ambae yeye anatarajiwa kuanza mazoezi mepesi siku ya jumatatu.

No comments