SINGIDA UNITED WASEMA HILI KUHUSU USAJILI WA DEUS KASEKE

Uongozi wa timu ya Singida United umesema kwamba kwa sasa bado hawajafanya mazungumzo na mchezaji wa timu ya Yanga,Deusi Kaseke kwa malengo ya kumsajili kama inavyoelezwa na wadau wa mpira wa miguu.

Katibu mkuu wa timu hiyo Abdulrahman Sima ameiambia MWANDIKE.BLOGSPORT kwamba ni kweli kocha mkuu wa klabu hiyo Hans van Der Plujim alitoa mapendekezo ya kumsajili kama kuna uwezekano lakini kwa upande wao kama uongozi hadi leo hii hawajafanya mazungumzo na mchezaji huyo.

Sima alisema kwamba kwa sasa bado wanaendelea na mchakato wa usajili kwa kufuata maagizo ya kocha mkuu hivyo pale watakapokamilisha usajili wa mchezaji yeyote basi uongozi hautosita kumtangaza.


No comments