TAIFA STARS KUANZA KUFANYA MAZOEZI USIKU
Timu ya mpira wa miguu ya Tanzania ‘Taifa Stars’inayodhaminiwa
na Bia ya Serengeti kutoka Kampuni ya Bia ya SBL, imesafiri salama kutoka Dar
es Salaam, Tanzania hadi hapa Alexandria, Misri.
Timu
iliyotumia Ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopia, ilipaa kutoka Dar es Salaam,
saa 10.45 jioni ambako ilipitia Addis Ababa kuunganisha ndege ya kufika Misri.
Stars
iliyokuwa na jumla ya watu 30 wakiwamo viongozi, benchi la ufundi na wachezaji
kwa ujumla, ilitua Uwanja wa Ndege ya Cairo, Misri majira ya saa 7.45 usiku
ambako mbali ya wenyeji Tolip Sports City, pia ilipokelewa na maofisa wa
ubalozi wa Tanzania walioko hapa Misri.
Baada
ya kupokelewa, timu hiyo ilisafiri kwa gari maalumu kutoka Cairo, Misri hadi
Alexandria umbali wa zaidi ya kilomita 180 na kufika alfajiri baada ya mwendo
wa takribani saa mbili. Saa za Misri na Tanzania zina tofauti ya dakika 60.
Misri wako nyuma kwa saa hiyo moja.
Kwa
niaba ya timu nzima, Kocha Mkuu, Salum Shabani Mayanga pamoja na viongozi
wengine akiwamo Mkuu wa Msafara, Wilfred Kidao walishukuru Mungu kwa kusafiri
salama hadi kufika hapa Alexandria kwa ajili ya kambi ya wiki moja kujindaa
kucheza na Lesotho. Pia walishukuru Watanzania wote kwa dua zao kwa kusafiri
salama.
Akizungumza
mara baada ya kukagua viwanja vya mazoezi leo asubuhi, Kocha Mayanga ambaye
alipewa majukumu ya kuifundisha timu hiyo mapema - Januari, mwaka huu, amesema:
“Programu ya mazoezi kwa timu hii itaanza leo saa 2.00 usiku. Ingawa siku
nyingine nitafanya asubuhi na jioni.”
Kwa
msingi huo, alisema kesho Alhamisi Juni mosi, atakuwa na mazoezi kwa vipindi
vyote viwili uwanjani - asubuhi na usiku kabla ya kutoa maelekezo darasani kwa
siku ya Ijumaa na baadaye mazoezi ya uwanjani tena.
Taifa
Stars inayopiga kambi hapa Misri, inajiandaa na mchezo dhidi ya Lesotho
utakaofanyika Juni 10, 2017 kwenye Uwanja wa Azam ulioko Chamazi nje kidogo ya
jiji la Dar es Salaam. Mchezo huo umepangwa kuanza saa 2.00 usiku.
Mchezo
dhidi ya Lesotho ni muhimu kwa Tanzania ikiwa ni mechi ya kwanza kwa Taifa
Stars katika Kundi ‘L’ kuwania nafasi muhimu ya kucheza fainali za Kombe la
Mataiafa ya Afrika (AFCON) za mwaka 2019 zitakazofanyika NCHINI Cameroon.
Mbali
ya Lesotho na Tanzania, mataifa mengine katika Kundi ‘L’ ni Uganda na Cape
Verde ambao pia wikiendi ya Juni 9, 10 na 11, mwaka huu watakuwa katika mchezo
wa kwanza pia kuwania nafasi hiyo.
Wachezaji wanaounda kikosi hicho cha Kocha Salum Mayanga
ni makipa Aishi
Manula (Azam FC), Benno Kakolanya (Yanga SC) na Said Mohammed
(Mtibwa Sugar).
Walinzi
wa pembeni wako Shomari Kapombe (Azam FC), Hassan Kessy
(Yanga SC), Mohammed Hussein (Simba) na Gadiel Michael.
Walinzi
wa kati ni Erasto Nyoni (Azam FC), Salim Mbonde (Mtibwa Sugar), Abdi
Banda (Simba SC) na Nurdin Chona (Tanzania Prisons) ilihali viungo wa kuzuia ni
Himid Mao (Azam FC) na Jonas Mkude kutoka Simba SC ambaye kwa sasa anapatiwa
matibabu baada ya kupata ajali.
Viungo
wa kushambulia Salum Abubakar (Azam FC), Said Ndemla (Simba SC) na
Mzamiru Yassin (Simba) wakati viungo wa pembeni ni Simon Msuva (Yanga SC),
Shizza Kichuya (Simba SC) na Farid Mussa (Teneriffe, Hispania).
Washambuliaji
wapo Mbwana Samatta (KRC Genk- Ubelgiji), Ulimwengu (AFC Eskilstuna – Sweden),
Ibrahim Ajib (Simba SC), Mbaraka Yusufu (Kagera Sugar) na Abdurahman Mussa
(Ruvu Shooting).
Wasaidizi
wa Mayanga katika benchi la ufundi ni Novatus Fulgence ambaye ni kocha msaidizi
Patrick Mwangata - kocha wa makipa pia yumo Meneja wa timu, Danny Msangi;
Mtunza Vifaa, Ally Ruvu, Daktari wa timu ni Richard Yomba na Daktari wa
viungo ni Gilbert Kigadye.
Post a Comment