JONAS MKUDE ANUSURIKA KIFO

Shabiki wa timu ya Simba aliyejulikana kwa jina la Shose amefariki dunia mapema leo hii baada ya ajali waliyopata maeneo ya Dumila wakitokea mkoani Dodoma walipokwenda kushuhudia mechi ya fainali ya kombe la FA iliyowakutanisha Simba na Mbao FC.

Taarifa zinaeleza kuwa miongoni mwa waliokuwemo kwenye gari hilo ni pamoja na kiungo wa Simba Jonas Mkude ambae kwa upande wake yeye amepata majeraha kidogo shingoni ambapo yeye na majeruhi wengine wamekimbizwa Hospitalini kwa ajili ya matibabu.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa baadhi ya wadau  wa Simba walisema kwamba Jonasi Mkude alikuwa anawai majukumu katika timu ya Taifa.

No comments