AVEVA AWAONGOZA MASHABIKI WA SIMBA KUWAGA MWILI WA SHOSE

Rais wa klabu ya Simba Evans Aveva leo hii amewaongoza mashabiki wa timu hiyo kuuaga mwili wa marehemu Shose Fidelis aliyefariki kwa ajali ya gali wakati akitokea mkoani Dodoma kushuhudia fainali ya michuano ya FA.

Aveva alisema kwamba kwa niaba ya uongozi na mashabiki kwa ujumla wamehudhunishwa na kifo cha shabiki huyo wa Simba kwani alikuwa ni miongoni mwa vijana ambao walikuwa na upendo wa dhati kwa timu hiyo.

Alisema kwamba kwa kutambua umuhimu wake watafanya jitihada kubwa timu ifanye vizuri ili waweze kumuenzi kutokana na mapenzi yake kwa klabu.


Nae msemaji wa timu ya Simba aliyefungiwa mwaka mmoja na TFF,Haji Manara ameelezea juu ya masikitiko yake juu ya kifo cha shabiki huyo akisema kwamba yeye ni miongoni mwa watu wa kwanza walioshuhudia tukio la kifo chake.

Manara alisema kwamba kifo cha Shose kimeacha pigo kubwa kwa klabu kwani ni miongoni mwa mashabiki ambao walikuwa na ushawishi mkubwa katika timu.

Aidha Manara alisema kwamba klabu kwa kushirikiana na wanachama wake wamekabidhi rambimbi ya shilingi milioni nne na laki mbili kwa ajili ya msiba huo na hii inatokana na kuguswa Zaidi na jambo hilo.

No comments