SINGIDA UNITED WAKILI KUFANYA MAZUNGUMZO NA AJIBU

Uongozi wa timu ya soka ya Singida United umesema kwamba bado hawajakamirisha usajili wa mchezaji Ibrahm Ajibu licha ya kuwepo kwa taarifa hizo.

Mwenyekiti wa Singida United Festus Sanga alisema kwamba ni kweli wapo kwenye mazungumzo na mchezaji huyo lakini bado hawajafanikiwa kukubaliana rasmi.

"Ni kweli tupo kwenye mazungumzo na Ajibu sisi kama Singida United tumempa ofa yetu lakini bado hakuna makubaliano rasmi kwani yule ni mchezaji mzuri na anawindwa na virabu mbalimbali,hivyo razima tuwe na subra"alisema Sanga.

Kwa upande mwingine Sanga alisema kwamba kwa sasa kikosi cha Singida United kipo jijini Dar es salaam chini ya kocha mkuu Hans van Der Pluijm kikiendelea na maandalizi kwa ajili ya kujiwinda na michuano ya SportPesa inayotaraji kuanza mwezi ujao.



No comments