JAMALI MALINZI ABADILI KANUNI YA LIGI

Rais wa shirikisho la mpira wa miguu hapa nchini TFF,Jamali Malinzi amesema kwamba kuna uwezekano mkubwa wa kanuni za uendeshaji wa mpira wa miguu msimu ujao zikabadilika ili kuendana nan chi zilizoendelea kisoka.

Akiongea mbele ya waandishi wa Habari leo hii Malinzi amesema kwamba moja ya kanuni inayotarajiwa kufanyiwa marekebisho ni pale timu zinapolingana pointi.

Malinzi alisema kwamba msimu ujao timu zikilingana pointi wataangalia namna ya timu hizo walipokutana katika ushiriki wa michezo yao ya ligi husika ili kupata bingwa.

Hata hivyo wazo hilo bado halijawa rasmi kwani limeonekana kupingwa na baadhi ya waandishi wa Habari wakidiliki kusema kuwa Rais wa TFF hakunukuu vizuri kipengele cha kanuni hiyo.

No comments