MWINYI HAJI NA AGREY MORIS WAONDOLEWA STARS

Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars leo hii kimeelekea nchini Misri kwa ajili ya kuweka kambi ya takribani siku saba ama nane kwa ajili ya maandalizi ya kusaka tiketi ya kucheza fainali za Afrika.

Akiongea mbele ya waandishi wa Habari leo hii kocha mkuu wa timu hiyo,Salum Mayanga amesema kwamba kwa ujumla maandalizi kwa upande wao tangu walipoingia kambini yamekuwa yakienda vizuri hivyo anaamini wataendelea kufanya vyema katika kambi ya nje.

Mayanga pia amewaondoa kikosini wachezaji wawili kutoka Zanzibar ambao ni Haji Mwinyi pamoja na Agrey Moris na nafasi zao kuchukuliwa na wacheji Gadiel Michael na mchezaji wa Tanzania Prisons Nurudin Chona..

Alisema kwamba sababu za kuwaondoa kikosini wachezaji hao ni kutokana na swala la uwanachama wa Zanzibar kutambuliwa na CAF kwa kipindi hiki baada ya kupata uwanachama kamili.

No comments