CHARLES MBUGE KUONGOZA KIKAO KUJADILI TAARIFA YA MALALE HAMSINI

Mwenyekiti wa timu ya Ruvu Shooting, Kanali wa Jeshi na Mkuu wa Kikosi cha Jeshi (CO) 832 Ruvu JKT, Charles Mbuge,leo hii anataraji kuongoza kikao cha viongozi wa timu kujadili taarifa ya Kocha Malale Hamsini aliyoiwasirisha baada ya ligi (VPL) msimu wa mwaka 2016/17 kumalizika.

Afsa Habari wa timu hiyo Masau Bwire amesema kwamba katika taarifa yake, pamoja na mambo mengine, Mwalimu Malale ameshauri wachezaji 10 kuachwa na wengine 6 kutoka klabu mbalimbali kuongezwa ili kukiimarisha kikosi msimu mpya wa ligi 2017/18.

Masau alisema kwamba dhamira yao ni kuona msimu ujao wanakiwa na kikosi bora ambacho kitaleta ushindani wa kweli kwenye ushiriki wa michezo ya ligi kuu ya Tanzania bara.

No comments