UWANJA WA MAO UTAKUWA HIVI BAADA YA KUMALIZA KAZI YAO KAMPUNI YA ZHENGTAR YA CHINA

Na: Sleiman ussi haji Zanzibar.
Jana Waziri wa Habari Utalii Utamaduni na Michezo Zanzibar Mh Rashid Ali Juma rasmi aliukabidhi Uwanja wa Mao Tse Tung kwa wakandarasi wa Kichina kampuni ya Zhengtar Group Company Limited kwaajili ya kuujenga kisasa uwanja huo ambao utajengwa kwa mwaka mmoja na miezi miwili.

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utalii Utamaduni na Michezo Omar Hassan Omar “King” amesema Uwanja huo utagharimu Shilingi Bilioni 12.5 kwa fedha za Tanzania ambapo Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China itatoa Shilingi Bilioni 11.5 huku Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itachangia zaidi ya Shilingi Bilioni 1 kati ya hizo Bilioni 12.5 ambazo watalipwa Wakandarasi wa uwanja huo ambao ni Kampuni ya Zhengtar Group Company Limited ambayo ina uzoefu mkubwa wa kujenga Viwanja wa Michezo.

Mhandisi wa uwanja huo Ali Mbarouk Juma amesema Ujenzi huo utakuwa na Viwanja viwili vya mpira wa miguu na chengine cha michezo ya ndani kama vile Mpira wa Kikapu, Mpira wa Mikono, Mpira wa Pete na mengineyo.
Katika Viwanja hivyo vya Mpira wa Miguu Mhandisi huyo amesema uwanja mmoja utakuwepo upande wa Magharibi ambao utakuwa na Jukwaa moja litakalochukuwa Mashabiki 1500 waliokaa.

Uwanja mwengine wa mpira wa miguu utakuwepo upande wa Mashariki ambao utakuwa na uwezo wa kuchukua Mashabiki waliokaa 900 katika jukwaa moja ambalo litakuwepo katika Uwanja huo.

Viwanja hivyo vitakuwa na taa ambazo zitaweza kuwezesha kuchezwa michezo hadi usiku.

No comments