UONGOZI YANGA WAWAOMBA RADHI MASHABIKI NA WANACHA KWA KIPIGO CHA 2-1

Uongozi wa klabu ya Yanga kupitia kwa katibu mkuu wa klabu hiyo Charse Boniphace Mkwasa umewaomba radhi wanachama na mashabiki wa timu hiyo kwa matokeo ya jumamosi dhidi ya Simba baada ya kufungwa kwa jumla ya mabao 2-1.

Mkwasa alisema kwamba kutokana na matokeo hayo klabu inawaomba kuwa watulivu katika kipindi hiki ambacho timu inakabiliwa na michuano mbalimbali ya ndani pamoja na ya kimataifa.

Aidha Mkwasa amewapongeza mashabiki wa timu hiyo kwa kuwa watulivu kwa dakika zote licha ya kupoteza mechi hiyo huku akiwasihi waendelee kuisapoti timu yao kwani bado wana matumaini ya kuwa mabingwa wa ligi kuu ya Tanzania bara.

No comments