MASHINDANO YA JUDO YA AFRIKA MASHARIKI NA KATI YAZINDULIWA RASMI LEO ZANZIBAR NA KUMALIZIKA KESHO
Na: Sleiman ussi haji, Zanzibar.
Mashindano ya Judo ya 11 ya Afrika Mashariki na kati yamezinduliwa rasmi asubuhi ya leo Jumamosi Machi 4 na kumalizika kesho Jumapili Machi 5 mwaka huu 2017 katika ukumbi wa Judo uliopo Amani Mjini Zanzibar.
Khamis Ali Mzee ambae ni katibu wa Baraza la Taifa la Michezo Zanzibar (BTMZ) ndie aliyezinduwa Mashindano hayo.
Katika mashindano 10 yaliopita, Zanzibar imewahi kuwa mwenyeji mwaka 2008 na 2013, hivyo mwaka huu ni mwaka wa tatu kwa Zanzibar kuwa mwenyeji wa Mashindano hayo makubwa ya Judo Afrika Mashariki na Kati ambayo kwa msimu huu yameshirikisha wachezaji kutoka nchi mbali mbali kama vile za Tanzania bara, Burundi, Kenya, Rwanda na Wenyeji Zanzibar.
Post a Comment