VICENT BOSSOU MBIONI KUJADILIWA

Uongozi wa klabu ya Yanga,umeweka bayana juu ya swala la mchezaji Vicent Bossou baada ya mchezaji huyo kuandika ujumbe katika mitandao kuwa anaidai klabu hiyo mshahara wa miezi 4.

Katibu mkuu wa klabu ya Yanga,Boniphace Mkwasa amesema kwamba  Bossou haidai klabu hiyo mishahara ya miezi minne kama habari zinavoenezwa.

"Cheki za mishahara ya beki huyo kwa siku 10 mwezi wa 12 na januar zilikwishaandaliwa na mtoa check amemueleza kujua kuchukua lakini sielewi kwa nini hakuzifuata"alisema Mkwasa.

Alisema kabla ya mechi na Simba SC alifanya vizuri mazoezi lakini kwa taarifa zilizopo aliondoka mazoezini bila ruksa ya mwalimu.

Hata hivyo Mkwasa amedai kuwa kwa sasa wanasubiri ripoti ya mwalimu kwa ajili ya kuchukua hatua juu ya swala hilo.

No comments