MALINZI APEWA JUKUMU LA KUSIMAMIA MADAWA YA KULEVYA

Kamishina wa kupambana na kuzibiti madawa ya kulevya Rogers Sianga amemuomba raisi wa shirikisho la mpira wa miguu hapa nchini Tff,Jamal Malinzi kuungana kwa pamoja katika kampeni ya kuzibiti matumizi ya madawa ya kulevya.

Sianga ameyasema hayo katika ziara ya timu ya vijana ya Serengeti boys ambayo Leo hii wametembelea kwenye kituo cha Sober House kinachojihusisha na huduma ya kutibu waathirika wa matumizi wa madawa hayo ya kulevya ambayo yamekuwa janga kubwa kwa nchi.

Alisema kwamba Malinzi ana fursa kubwa ya kusimamia swala hilo na likafika kwa walengwa kwani usimamizi wake katika mpira wa miguu una tija kubwa.

"Nakuomba Raisi wewe una nafasi kubwa ya kuelimisha jamii juu ya swala hili kwani una nafasi kubwa sana ya kupata nafasi ya kuzungumza na uma ukakusikiliza tofauti na mimi ambae sipati fursa za mara kwa mara kuzungumza na jamii hapa kwenye nishukuru huu mwaliko wa mkurugenzi wa Sober House ndie ikatokea mimi kupata nafasi hii"alisema Sianga.

No comments