YANGA WALIKUWA MTU 10 TANGU DK YA 5

NA;DEOGRATIUS VAN MGINA

Pambano la watani wa jadi Simba na Yanga limemalizika siku ya jana ya tarehe 25 ya mwezi wa pili na mamia ya mashabiki wa soka wakishuhudia wekundu wa Msimbazi Simba wakiibuka na ushindi wa mabao 2-1 tena wakiwa pungufu uwanjani tangu dakika ya 55 ya mchezo.

Baada ya mpambano huo shangwe kwa mashabiki wa Simba ziliendelea kutawala kwa kuridhishwa na kiwango cha wachezaji wao wakitoka nyuma kwa bao moja na kufanikiwa kupata ushindi wa mabao 2-1.

Kama ilivyo ada kwa watanzania ama wapenda soka baada ya mechi ya dabi huwa kuna mengi yanazungumzwa,nami kwa mtazamo wangu siko kando na swala hili la kuzungumzia pambano la Simba na Yanga ambalo limekuwa gumzo kila pembezoni mwa nchi.

Mtazamo wangu mimi unalenga sehemu saba ambazo nimeziona kwa pande zote mbili kwa kile kilichofanyika uwanjani.

1.Omog alichemka kwenye uchaguzi wake wa kikosi cha kwanza na bahati nzuri alirekebisha makosa mapema niliona kabisa kosa la kumuweka Liuzio ili hali hakuna alichoonesha tangu atue Simba.

2.Lwandamina alipiga hesabu zake vizuri sana bahati mbaya wachezaji wake wakaenda kuzivuruga baada ya kupata goli wakaanza kucheza kimadaha na kusahau kuwa game haijaisha ubovu wa Lwandamina hana mawasiliano na wachezaji wake wakiwa katika Pitch anamtindo wa kutulia kama Van Gaal na hata aliposimama ndo alivuruga zaidi kikosi bora angesimama Mwambusi.

3.Ubora wa Simba katika mchezo wa jana umekuja kutokana na aina ya wachezaji alionao ambao wengi bado ni vijana na wana njaa kweli.... Walikuwa na stamina kuliko wa Yanga ambao walivurugika katikati baada ya Ndemla kuingia na Kamusoko kutoka na hasa pale na Mkude alipoongezeka.
 
4.Simba walimiliki sana mpira baada ya Red card kwa Bokungu kwa kuwa walikuwa na viungo wengi na wachezaji wenye kasi na uwezo wa kumiliki mpira na walicheza zaidi ya uwezo wao kwakuwa walijua wapo pungufu....Mkude, Ndemla,Muzamiru na Kotei wakatulia katikati huku Kichuya na Ajib wakicheza kwenye mashavu ya ushambuliaji na wakati mwingine kurudi kwenye fullbacks... Kwenye Central back akabaki Banda huku mara moja moja Zimbwe akisogea kati kumsaidia pale kwenye CS akabaki Mavugo na bahati mbaya wachezaji wa Yanga pumzi ilikuwa ishakata.

5.Wengi wanailaumu defence ya Yanga hasa katika goli la kwanza ni sahihi lakini kosa kubwa la Dante la kuuacha mpira upite kichwani mwake na kumkuta Mavugo lilikuwa kubwa zaidi huenda ufupi wake ulichangia lakini wakati huo kiungo cha Yanga kilikuwa kimekufa na hiyo ilitokana labda na kucheza kwa lengo la kuzuia sana wakiamini wadhashinda na Simba pungufu haiwezi kuchomoa bahati mbaya hawakuangalia aina ya wachezaji walioingia upande wa Simba hasa Kichuya & Mkude ambao walikuwa moto..... Kuruhusu mashambulizi langoni mwao kuliwasogeza zaidi Simba na kuwafanya wajiamini zaidi licha ya kuwa wachache.
 
6.Simon Msuva huyu jana hakuwa mchezoni kabisa alistahili kutoka mapema lakini goli lake la mapema likaficha udhaifu wake uliokuwa ukimfanya hata Tambwe asionekane pale.. Huenda lile goli la mkwaju alilofunga liimfanya alirelax na kuona ashamaliza kazi nathubutu kusema huyu ndie aliowavuruga Tambwe na Chirwa pale mbele .....naweza sema Yanga walikuwa mtu 10 tangu baada ya goli la Penati Msuva hakuwepo uwanjani labda akili yake ilikuwa ianendelea kushangilia goli.

7.Nina mashaka sana na ubora wa Lwandamina sijaona alichoongeza ndani ya Yanga zaidi ya kuirudisha nyuma labda bado anajenga timu lakini ana kazi nzito sana na siajabu ukisikia Pluijm anarejeshwa.

No comments