SIMBA WAAMUA KUMUOMBA RADHI RAISI WA NCHI JOHN POMBE MAGUFULI


Uongozi wa klabu ya Simba kupitia kwa Raisi wa klabu hiyo Evansi Aveva umemuomba radhi Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli kufuatia mashabiki wa klabu hiyo kufanya uharibufu katika uwanja wa Taifa baada ya kung’oa viti Zaidi ya 1781 kwenye pambano la watani wa Jadi lililofanyika siku ya jumamosi.

Akiongea mbele ya waandishi wa Habari leo hii,mkuu wa idara ya mawasiliano wa klabu hiyo Haji Manara amesema kwamba uongozi kwa kushirikiana na benchi la ufundi pamoja na wanachama wa klabu hiyo wameendelea kuchukua hatua ya kuomba radhi hadi kwa Raisi baada ya kuchukizwa na hatua zilizofanywana na mashabiki wake ambao si za kiungwana.

Amesema kwamba kwa upande wao uongozi unaomba radhi kwa Raisi wa nchi kwa kua yeye ndie mtendaji mkuu wa mali za wananchi hivyo kupitia kwake pamoja na waziri mwenye dhamana ya michezo wanaamini huenda wakabatilisha maamuzi yao ya kuwazuia kutumia uwanja wa Taifa.

No comments