SERIKALI YAZIPIGA MARUFUKU SIMBA NA YANGA KUUTUMIA UWANJA WA TAIFA


Serikali kupitia kwa wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo imezipiga marufuku Yanga na Simba kuutumia uwanja wa Taifa katika michezo yao mbalimbali kufuatia vurugu zilizofanywa na mashabiki wa Simba hapo jana katika mchezo wa ligi kuu ya Tanzania bara uliyowakutanisha mahasimu hao.

Akiongea mbele ya waandishi wa Habari leo Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Nape Nnauye amesema kwamba nivyema klabu hizo zikatafuta viwanja vya kutumia kuliko kuhalibu uwanja huo wa Taifa ambao ni mali ya watanzania kupitia kodi zao wanazotoa.

Amesema kwamba kitendo ambacho kimefanywa na mashabiki cha kung'oa viti si cha kiungwana na kinastahili kukemewa kwani aileti tija katika maendeleo ya mpira wa miguu hapa nchini.

"Uwanja huu hautatumika kwa Yanga na Simba mpaka tutakapoamua vingenevyo hapo baadae hawatatumia uwanja labda watafute viwanja vingine kwa sababu hapa kuna pesa za walipa kodi kuna pesa za watanzania na wanaotakiwa kuutumia uwanja huu ni wengi kuliko Yanga na Simba wako wengeni kwa kweli ni wastarabu wanaweza kuutumia uwanja huu"alisema Nape.

No comments