ZFA WAIKUBALIA YANGA KUUTUMIA UWANJA WA AMANI

Chama cha soka visiwani Zanzibara ZFA kimesema kwamba kimepokea nakala ya barua kutoka katika uongozi wa klabu ya Yanga ukitaka kuutumia uwanja wa Taifa wa Zanzibar wa Amani katika michezo ya ligi kuu ya Tanzania bara.

Katibu mkuu wa ZFA Khasim Haji Salum amesema kwamba kwa upande wao kama uongozi  umekubaliana na jambo hilo lakini maamuzi kamili ya kuruhusiwa uwanja huo ni jukumu la Serikali ambao wao ndio wenye mamlaka kamili.

Amesema kwamba hatua ambayo imechukuliwa na klabu ya Yanga ya kutaka kuutumia uwanja wa Amani kwa upande wao kama ZFA wameridhishwa na maamuzi hayo na kwa upande wao hawana kikwazo chochote juu ya ujio wao kwani itawapa fursa mashabiki wa Yanga visiwani humo kuiona timu yao ikicheza katika michezo ya ligi kuu ya Tanzania bara kupitia uwanja huo.

"Kiukweli kama sisi ZFA tumekubaliana na jambo hilo kwani litawapa fursa mashabiki wa Yanga hapa Zanzibar kuiona timu yao kwani hapa kuna mashabiki wengi wa Yanga hivyo kuja kwao hapa litakua jambo la faraja kwao"alisema Khasim.

No comments