ABDUL MOHAMED AWA MENEJA MKUU WA AZAM FC

Uongozi wa klabu y Azam FC ya jijini Dar es salaam leo hii umemtamburisha rasmi Abdul Mohamed kuwa ndie meneja mkuu wa timu hiyo kwa sasa atakayehusika kuratibu mambo mbalimbali ya klabu.

Akiongea mbele ya waandishi wa Habari wakati wa utamburisho huo mtendaji mkuu wa klabu hiyo Saad Kawemba amesema kwamba kuwepo kwake Abdul Mohamed ndani ya timu anaamini atawasaidia kuleta chachu ya maendeleo kwa upande wao hasa kupitia ujuzi wake aliokuwa nao.

Nae Abdul Mohamed amesema kwamba kuwepo kwake ndani ya klabu hiyo ya Azam atahakikisha kuwa analeta tija ya maendeleo ya mpira wa miguu hapa nchini na nia yake ni kuona timu hiyo inakua tofauti na timu nyingine.

Amesema kwamba kwanza amefarijika kupata nafasi hiyo adhimu kwake hii inatokana na viongozi kutambua mchango wake katika maendeleo ya mpira wa miguu hivyo kutokana na jambo anaamini kwa kushirikiana na viongozi pamoja na mashabiki wa klabu hiyo na wadau wengine anaamini Azam itakua na mafanikio makubwa ya kiundeshaji.

No comments