NAPE APONGEZA MFUMO MPYA WA UUZAJI WA TIKETI

Serikali kupitia Wizara ya Habari imeridhishwa na mfumo wa matumizi ya tiketi za mtandao ambao umetumika katika pambano la watani wa jadi Simba na Yanga lililomalizika kwa timu hizo kufungana bao 1-1.

Akiongea mbele ya waandishi wa Habari,waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Nape Nnauye amesema kwamba mfumo huo ambao unaendeshwa na kampuni ya Selcom umeonyesha kuleta matumaini kwani kwa mara ya kwanza umeonyesha mwanga tena katika mechi kubwa na yenye ushindani.

Amesema kwamba ingawa kuna changamoto ambazo zimeonekana lakini kwa kiasi kikubwa mfumo huo umefanikiwa na amewataka watanzania waendelee kuunga mkono mfumo huo na kwa upande wao watayafanyia kazi mapungufu ambayo yamejitokeza kwa kushirikiana na kampuni husika ya Selcom.

Hata hivyo Nape amewataka mashabiki wa mpira wa miguu hapa nchini kuacha tabia ya mazoea katika michezo kwani inasikitisha mtu kushindwa kuingia kwenye geti ambalo halina foleni eti kisa si geti ambalo limezoeleka kuingia na mashabiki wa timu yake anayoipenda.

"Ujue mashabiki sijui wakoje mfano mzuri katika ile mechi kuna mageti kulikua hakuna msongamano wa watu lakini nashangaa kuona hao hao mashabiki wanajazana sehemu moja  yenye msongamano huku wakiacha sehemu ambayo haina mashabiki na mashine zilikua zinfanya kazi kwa haraka zaidi"alisema Nape.

No comments