BARAZA LA MICHEZO TANZANIA LIMETANGAZA KUTOTAMBUA UKODISHWAJI WA YANGA

Baraza la michezo hapa nchini BMT kupitia kwa katibu mkuu baraza hilo Mohamed Kiganja limetangaza kutotambua ukodishwaji wa klabu ya Yanga kwa kampuni iliyopewa jina la Yanga yetu kwa kuwa ukodishwaji huo haukufuata taratibu na misingi ya kanuni ya klabu hiyo.

Akiongea mbele ya waandishi wa Habari leo hii, Kiganja amesema kwamba hatua hiyo iliyofanywa na viongozi wa Yanga chini ya mwenyekiti wa klabu Yusuphu Manji imeenda kinyume na katiba ya klabu.

"Taarifa nilizonazo sheria ya muungano ya wadhamini sura ya 318 ya mwaka 2002  imeeleza wazi vilabu hivi vina bodi ya wadhamini lakini wametuelekeza sisi kwamba pamoja na kukutajia majina lakini wametueleza kua bodi ya wadhamini wa klabu ya Yanga ni bodi ya mpito ambayo wanataka kuifuta sasa bodi ya mpito haiwezi kufanya maamuzi makubwa ambayo watanzania zaidi ya milioni tatu waamuliwe na watu ambao hawajapata ridhaa ya wanachama"alisema Kiganja.

Kiganja amesema kwamba klabu hiyo kwa sasa haina baraza hai la wadhamini kwani muda wao umeshaisha hivyo anashangaa kuona baraza hilo linachukua jukumu la kuikodisha timu ikiwa wao wenyewe kwa sasa hawana sifa za kuwa wadhamini wa klabu hiyo yenye maskani yake mitaa ya Jangwani jijini Dar es Salaam.

No comments