STARS YAISURUBU DR CONGO

Na Said Ally
Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) Leo hii imefanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 2-0 dhidi ya DR Congo katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki uliochezwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Mechi hiyo ambayo ilikuwa na ushindani wa hali ya juu,kipindi cha kwanza timu zote zilikwenda vyumbani pasipo kufungana.

Katika kipindi cha pili timu zote zilirejea uwanjani kwa Kasi kubwa lkn Dr Congo walionekana kucheza kwa tahadhari kubwa kwa kufanya mashambulizi zaidi kwenye lango la Stars,lkn mashambulizi hayo hayakuweza kuleta athari kwa Stars.

Kocha Salum Mayanga alifanya mabadiliko katika kipindi hicho cha pili kwa kumtoa Mohammed Issa na nafasi yake kuchukuliwa na Ibrahim Ajibu ambapo mabadiliko hayo yalileta tija kwa Stars,kwani kunako dk ya 31 Mbwana Samatta alifanikiwa kuiandikia Stars bao la kuongoza baada ya kupokea pasi nzuri ya Shiza Kichuya.

Shiza Kichuya akionekana kucheza kwa juhudi na maarifa alifanikiwa kuifungia Taifa Stars bao la pili kunako dakika ya 88 ya mchezo akipokea krosi nzuri ya Mbwana Samatta.

Baada ya bao hilo Kichuya alitolewa nje na nafasi yake kuchukuliwa na mchezaji Rashidi Mandawa ambae nae alionekana kuiongezea nguvu zaidi Star kulinda ushindi huo wa mabao 2-0.

Hadi dakika 90 zinamalizika Taifa Stars ilifanikiwa kuibuka na ushindi huo wa mabao 2-0,ushindi ambao umewafurahisha mashabiki wengi waliojitokeza katika uwanja wa Taifa.

No comments