MCHEZO WA SIMBA NA YANGA WAPANGIWA TAREHE
Na Said Ally
Mechi ya ligi kuu ya Tanzania bara itakayowakutanisha watani wa jadi Simba na Yanga imepangwa kuchezwa April 29 mwaka huu kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Akiongea mbele ya waandishi wa Habari hii Leo,mtendaji mkuu wa bodi ya ligi Boniphace Wambura alisema kwamba mechi hiyo imepangwa kuchezwa tarehe hiyo baada ya tarehe ya awali iliyopangwa ya March 7 mwaka huu Yanga kuwa na mchezo wa kimataifa wa kombe la shirikisho barani Afrika.
Mbali na mechi hiyo pia bodi ya ligi imezipangia tarehe mechi za viporo ikiwemo mechi ya Njombe Mji na Simba ambayo Sasa imepangwa kuchezwa April 3 mwaka huu huko Njombe.
Aidha Wambura alisema kwamba ratiba hiyo inaweza ikawa na mabadiliko siku zijazo kutokana na ushiriki wa Yanga katika michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika kama itafanikiwa kuingia hatua ya makundi.

Post a Comment