YONDANI NA WENZAKE WAENDA MOROGORO

Na Said Ally
Wachezaji wanne wa timu ya Yanga ambao walikuwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) mchana huu wameelekea mkoani Morogoro kwa ajili ya kuungana na wenzao kuendelea na mazoezi ya kujiwinda na mechi ya FA dhidi ya Singida United.

Wachezaji hao ni pamoja na Kelvin Yondani,Gadiel Michael,Hassani Kessy na Ibrahim Ajibu.

Ramadhani Kabwili yeye ameshindwa kuungana na wenzake kwenda mkoani Morogoro kwa kuwa amejiunga na timu ya Taifa ya vijana ya Ngorongoro Heroes iliyo kambini ikijiandaa na mchezo wa kimataifa.

Mbali na wachezaji hao pia katika msafara huo yumo kocha msaidizi Noel Mwandila ambae nae alikuwa bado hajajiunga na kikosi hicho kwenye kambi hiyo ya mkoani Morogoro.

Yanga inataraji kucheza na Singida United April 1 mwaka huu kwenye uwanja wa Namfua mkoani Singida ukiwa ni mchezo wa robo fainali ya michuano ya kombe la Azam Sports Federation.

No comments