NJOMBE MJI YASEMA BORA KUPOTEZA MECHI YA FA KULIKO KUFUNGWA NA SIMBA

Na Said Ally
Nusu ya wachezaji wa timu ya Njombe Mji wameshindwa kuambatana na timu kuelekea mkoani Shinyanga kucheza mechi ya FA dhidi ya Stand United hii leo jambo ambalo limepelekea timu hiyo kufungwa kwa jumla ya bao 1-0.

Akiongea na MWANDIKE.BLOGSPOT,katibu mkuu wa timu hiyo Obeid Mwakasungula alisema kwamba kupoteza kwao mchezo wa leo kumetokana na kutokuwa na maandalizi mazuri kwa upande wao hasa kubanwa na ratiba.

Mwakasungula alisema kwamba iliwalazimu kusafiri na kikosi cha wachezaji 13 kwenda Shinyanga na kuwaacha wachezaji wengine Njombe ili wapate muda mzuri wa kujiandaa na mechi dhidi ya Simba kwani ratiba haikuwa rafiki kwa upande wao.

Alisema kwamba uongozi ulikubaliana kuwa ni vyema wakaweka mkazo kwenye mechi za ligi ikiwemo ya Simba itakayopigwa April 3 mwaka huu ili kujiweka kwenye mazingira mazuri ya kutoshuka daraja.

Aidha aliongeza kwa kusema kuwa haya yote yametokana na upangaji mbovu wa ratiba jambo ambalo limewaweka katika wakati mgumu kushindwa kujipanga vyema kwenye mechi yao ya FA pamoja na ya ligi kuu ya Tanzania bara.

No comments