STARS IKO TAYARI KUWAVAA DR CONGO

Na Said Ally
Kocha msaidizi wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) Hemed Morocco amesema kwamba kikosi cha timu hiyo kimejiandaa vyema kuwakabili DR Congo hapo kesho katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki utakaopigwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Akiongea mbele ya Waandishi wa Habari hii leo Morocco alisema kwamba ukiwaondoa Aishi Manula na Abdulazizi Makame ambao ni majeruhi wote waliosalia wako vizuri kwa ajili ya pambano hilo litakaloanza kunako mishale ya saa 10 jioni.

Alisema kwamba mechi ya kesho ni ngumu lakini hawako tayari kupoteza kwa mara nyingine kwani nia yao ni kushinda ili kujiweka kwenye mazingira mazuri katika ubora wa viwango vya FIFA na pia kujiandaa vyema na mashindano ya kusaka tiketi ya kucheza fainali za Afrika za mwaka 2019 nchini Cameroon.

No comments