MKUTANO MKUU WA YANGA KUFANYIKA MWEZI MEI

Na Mwandishi Wetu Timu ya Yanga inatarajiwa kufanya Mkutano wake Mkuu wa mwaka Mei 5 mwaka huu katika ukumbi utakaotajwa baadaye mjini Dar es Salaam.

Mkutano huo ni matokeo ya kikao cha Kamati ya Utendaji ya Yanga kilichofanyika Jumapili iliyopita mjini Dar es Salaam chini ya Kaimu Mwenyekiti, Clement Sanga ambacho kimewataka wanachama kujindaa kwa ajenda zitakazotangazwa baadaye.


Akiongea mbele ya waandishi wa Habari Katibu Mkuu wa Yanga SC, Charles Boniface Mkwasa amesema kwamba mkutano huo utakuwa maalum kwa wanachama kujadili masuala mbalimbali na kwa ujumla mustakabali wa klabu.


Awali klabu hiyo ilitaka kufanya mkutano huo mwezi February lakini ilishindikana baada ya uongozi kudai kuwa nilikuwa na taratibu ambazo zilikuwa hajakamilika.

No comments