YANGA KUANZA UGENINI NA TIMU YA DARAJA LA PILI

Na,Said Ally
Timu ya soka ya Yanga imepangwa kucheza na timu ya Ihefu FC ya mkoani Mbeya katika mchezo wa kombe la Azam Sport Federation baada ya droo ya raundi ya tatu kupangwa leo hii.

Yanga itacheza mchezo huo ikiwa ugenini huko mkoani Mbeya na timu hiyo ya Ihefu FC ambayo inashiriki ligi daraja la pili.

Wababe wa Simba,timu ya Green Warriors watapepetana na Singida United ambapo Singida United itawalazimu kuanzia ugenini kwenye pambano hilo ambalo linatarajiwa kuwa na ushindani wa hali ya juu.

Mechi nyingine ni pamoja na

KMC VS Toto Africans
Njombe Mji VS Rhino Rangers
Kiluvya United VS JKT Oljoro
Ndanda VS Biashara United
Pamba VS Stand United
Tanzania Prisons VS Bukina Faso
Polisi Tanzania VS Friends Rengers
JKT Tanzania SC VS Polisi Dar
Majimaji VS Ruvu Shooting
Mwadui FC VS Dodoma FC
Kariakoo Lindi VS Mbao FC
Majimaji Rengers VS Mtibwa Sugar
Kagera Sugar VS Buseresere FC
Shupavu VS Azam FC

No comments